Walengwa wa Ujumbe katika Bembelezi za Watikuu
Loading...
Date
2022-08
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Journal of Swahili Studies
Abstract
Nyimbo zikiwa za watoto, inatarajiwa kuwa walengwa watakuwa watoto wenyewe kwa kuwa maudhui yaliyomo yatawalenga. Bembelezi zilizotafitiwa katika tamaduni mbalimbali ulimwenguni zinaonyesha kuwa ujumbe uliyomo huwalenga watoto na wakati mwingine, mama na baba zao. Kimsingi, wanawake, kando na kuzitumia katika shughuli za kubembeleza watoto, huzitumia pia kama jukwaa la kujieleza na kutakasa mioyo yao kutokana na uchungu, mtamauko na mfadhaiko wa mawazo uliosababishwa na matatizo ya kindoa kutokana na mifumo ya kibabedume inayoendelezwa katika baadhi ya jamii. Makala hii inachunguza diskosi zinazojitokeza katika bembelezi za Watikuu ili kubaini walengwa wa ujumbe uliomo. Lugha inayotumiwa na wanawake katika uimbaji wa bembelezi hizi inatilia shaka iwapo ujumbe uliomo unalenga tu watoto au mna watu wengine wanaolengwa kando na watoto
Description
Journal Article
Keywords
Bembelezi, Walengwa, Washiriki, Ujumbe, Watikuu
Citation
Akaka, L., & Simwa, S. W. (2022). Walengwa wa Ujumbe katika Bembelezi za Watikuu. East African Journal of Swahili Studies, 5(1), 288-296. https://doi.org/10.37284/jammk.5.1.817.